18 Sasa Yuda akamkaribia, akamwambia: “Nakuomba, bwana wangu, tafadhali mruhusu mtumwa wako aongee neno masikioni mwa bwana wangu,+ wala usiache hasira+ yako iwake juu ya mtumwa wako, kwa sababu wewe ni kama Farao.+
8 Basi sasa si ninyi ambao mlinileta hapa,+ ila ni Mungu wa kweli, ili aniweke niwe baba+ kwa Farao na bwana kwa nyumba yake yote na kuwa mtawala katika nchi yote ya Misri.
10 naye akamkomboa kutoka katika dhiki zake zote na kumpa neema na hekima machoni pa Farao mfalme wa Misri. Naye akamweka aongoze Misri na nyumba yake yote.+