6 Basi sasa njoo, tafadhali; uwalaani+ watu hawa kwa ajili yangu, kwa maana ni wenye nguvu kuliko mimi. Huenda nitaweza kuwapiga nami niwafukuze kutoka katika nchi; kwa maana najua vema kwamba yule unayembariki ni mtu aliyebarikiwa naye yule unayemlaani, amelaaniwa.”+
10 Ndipo hasira ya Balaki ikawaka juu ya Balaamu naye akapiga makofi,+ naye Balaki akamwambia Balaamu: “Nilikuita ili uwalaani+ adui zangu, na, tazama! umewabariki kabisa mara hizi tatu.