2 Ndipo suria wake akaanza kufanya uasherati+ dhidi yake. Mwishowe suria huyo akamwacha, akaenda nyumbani kwa baba yake huko Bethlehemu katika Yuda, akaendelea kukaa huko miezi minne kamili.
25 Lakini wanaume hao hawakutaka kumsikiliza. Basi mtu huyo akamchukua suria+ wake na kumleta kwao nje; nao wakaanza kulala na mwanamke huyo,+ wakaendelea kumtendea vibaya+ usiku wote mpaka asubuhi, kisha wakamwacha aende wakati wa mapambazuko.