35 Naye akatuma wajumbe+ katika Manase yote, nao pia wakakusanywa pamoja kumfuata. Pia akatuma wajumbe kotekote katika Asheri na Zabuloni na Naftali, nao wakaja kukutana naye.
33 Wa Zabuloni+ wale wanaoingia jeshini, wanaojipanga kivita pamoja na silaha zote za vita, walikuwa 50,000, nao wakawa wakimiminika kwa Daudi bila kuwa na mioyo miwili.