-
Yoshua 10:3-5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Basi Adoni-sedeki mfalme wa Yerusalemu akatuma ujumbe huu kwa Hohamu mfalme wa Hebroni,+ Piramu mfalme wa Yarmuthi, Yafia mfalme wa Lakishi, na kwa Debiri mfalme wa Egloni:+ 4 “Njooni mnisaidie kuwashambulia wakaaji wa Gibeoni, kwa sababu wamefanya amani na Yoshua na Waisraeli.”+ 5 Ndipo wafalme watano wa Waamori,+ yaani, mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Egloni wakakusanyika pamoja na majeshi yao, wakaenda kupiga kambi ili kulishambulia jiji la Gibeoni.
-