54 Haya ndiyo yaliyokuwa makao yao kulingana na kambi zao katika eneo lao: wazao wa Haruni waliokuwa wa ukoo wa Wakohathi, waliangukiwa na kura ya kwanza, 55 waliwapa Hebroni+ katika nchi ya Yuda, pamoja na malisho yake. 56 Lakini mashamba ya jiji na vijiji vyake walimpa Kalebu+ mwana wa Yefune.