Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hesabu 21:21-26
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 21 Sasa Waisraeli wakawatuma wajumbe wakamwambie hivi Sihoni mfalme wa Waamori:+ 22 “Turuhusu tupite katika nchi yako. Hatutageuka na kuingia katika mashamba yenu au shamba lolote la mizabibu. Hatutakunywa maji ya kisima chochote. Tutafuata Barabara ya Mfalme mpaka tutakapokuwa tumepita katika eneo lako.”+ 23 Lakini Sihoni hakuwaruhusu Waisraeli wapitie katika eneo lake. Badala yake, Sihoni akawakusanya watu wake wote kwenda kuwashambulia Waisraeli nyikani, akafika Yahazi na kuanza kupigana nao.+ 24 Lakini Waisraeli wakamshinda kwa upanga+ na kumiliki nchi yake+ kuanzia Arnoni+ mpaka Yaboki,+ karibu na Waamoni, kwa sababu jiji la Yazeri+ linapakana na eneo la Waamoni.+

      25 Basi Waisraeli wakachukua majiji hayo yote, wakaanza kuishi katika majiji yote ya Waamori,+ huko Heshboni na miji yake yote. 26 Kwa maana Heshboni lilikuwa jiji la Sihoni, mfalme wa Waamori ambaye alikuwa amepigana na mfalme wa Moabu na kuchukua nchi yake yote mpaka Arnoni.

  • Kumbukumbu la Torati 2:26, 27
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 26 “Kisha kutoka katika nyika ya Kedemothi,+ niliwatuma wajumbe kwa Mfalme Sihoni wa Heshboni, ili wampe ujumbe huu wa amani:+ 27 ‘Niruhusu nipite katika nchi yako. Nitatembea barabarani tu, sitakwenda kulia wala kushoto.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki