-
Waamuzi 3:28Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
28 Ndipo akawaambia, “Nifuateni, kwa sababu Yehova amewatia maadui wenu, Wamoabu, mikononi mwenu.” Nao wakamfuata, wakateka vivuko vya Yordani ili kuwazuia Wamoabu wasikimbie, na hawakumruhusu mtu yeyote avuke.
-
-
Waamuzi 7:24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 Gideoni akatuma wajumbe katika eneo lote lenye milima la Efraimu, akisema, “Shukeni mkawashambulie Wamidiani, wazuieni wasivuke vijito vyote vya maji kufikia Beth-bara na pia Yordani.” Basi watu wote wa Efraimu wakakusanyika pamoja, nao wakawazuia kuvuka vijito vyote vya maji kufikia Beth-bara na Yordani.
-