-
Mwanzo 18:7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
7 Kisha Abrahamu akakimbia kwenda kwenye mifugo, akachagua ng’ombe dume mchanga, mzuri na laini. Akampa mtumishi wake, naye akafanya haraka kumtayarisha.
-
-
Waamuzi 6:18, 19Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
18 Tafadhali usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea zawadi yangu na kuiweka mbele yako.”+ Basi akasema, “Sitaondoka mpaka utakaporudi.” 19 Kwa hiyo Gideoni akaingia nyumbani na kutayarisha mwanambuzi na kuoka mikate isiyo na chachu kwa kutumia efa* ya unga.+ Akaweka nyama katika kikapu na kutia mchuzi katika chungu cha kupikia; kisha akampelekea chini ya ule mti mkubwa.
-