-
Waamuzi 14:8, 9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Baadaye alipokuwa akirudi kumchukua mwanamke huyo aende naye nyumbani,+ alienda kuangalia ule mzoga wa simba, nao ulikuwa na nyuki wengi na asali. 9 Basi akakwangua asali hiyo na kuitia mikononi mwake, akaila huku akitembea. Alipomfikia baba yake na mama yake, akawagawia ili wale. Lakini hakuwaambia kwamba aliikwangua kutoka katika mzoga wa simba.
-