-
Yoshua 19:47, 48Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
47 Lakini eneo la kabila la Dani halikuwatosha kwa sababu lilikuwa dogo.+ Basi wakaenda kushambulia jiji la Leshemu,+ wakaliteka na kuwaangamiza wakaaji wake kwa upanga. Wakalimiliki na kukaa ndani yake, kisha wakabadili jina Leshemu kuwa Dani, jina la babu yao.+ 48 Huo ndio uliokuwa urithi wa kabila la Dani kulingana na koo zao. Hayo ndiyo yaliyokuwa majiji na vijiji vyake.
-
-
1 Wafalme 4:25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Watu wa Yuda na Israeli waliishi kwa usalama, kila mtu chini ya mzabibu wake mwenyewe na chini ya mtini wake mwenyewe, kuanzia Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.
-