8 Wakaulizana, “Ni kabila gani la Israeli ambalo halikufika Mispa mbele za Yehova?”+ Wakagundua kwamba hakuna yeyote kutoka Yabesh-gileadi aliyekuja kambini kukusanyika na Waisraeli wengine.
12 Miongoni mwa wakaaji wa Yabesh-gileadi walipata mabikira 400 ambao hawajawahi kufanya ngono na mwanamume. Basi wakawaleta kambini huko Shilo,+ katika nchi ya Kanaani.