Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Wafalme 9:1-3
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Kisha nabii Elisha akamwita mmoja wa wana wa manabii na kumwambia: “Jifunge mavazi yako kiunoni, na uchukue haraka chupa hii ya mafuta uende Ramothi-gileadi.+ 2 Utakapofika huko, mtafute Yehu+ mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi; ingia ndani, umchukue kutoka miongoni mwa ndugu zake, na kumpeleka katika chumba cha ndani zaidi. 3 Kisha chukua chupa ya mafuta, uyamimine juu ya kichwa chake na kusema, ‘Yehova anasema hivi: “Ninakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.”’+ Halafu ufungue mlango na kukimbia bila kukawia.”

  • 2 Wafalme 9:30-33
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 30 Yehu alipofika Yezreeli,+ Yezebeli+ akasikia habari hizo. Basi akapaka macho yake wanja na kupamba nywele zake, akatazama chini kupitia dirishani. 31 Yehu alipokuwa akiingia langoni, Yezebeli akasema: “Je, mambo yalimwendea sawa Zimri, aliyemuua bwana wake?”+ 32 Yehu akatazama juu dirishani na kuuliza: “Ni nani aliye upande wangu? Ni nani?”+ Mara moja maofisa wawili au watatu wa makao ya mfalme wakamtazama wakiwa dirishani. 33 Yehu akasema: “Mtupeni chini mwanamke huyo!” Kwa hiyo wakamtupa chini, na kiasi fulani cha damu yake kikatapakaa kwenye ukuta na farasi, kisha Yehu akamkanyaga-kanyaga.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki