Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Mambo ya Nyakati 25:20-24
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 20 Lakini Amazia hakusikiliza,+ kwa sababu Mungu wa kweli alikusudia kuwatia mikononi mwa adui,+ kwa sababu walikuwa wameifuata miungu ya Edomu.+ 21 Basi Mfalme Yehoashi wa Israeli akapanda kwenda huko, naye akapambana vitani na Mfalme Amazia wa Yuda huko Beth-shemeshi,+ jiji la Yuda. 22 Watu wa Yuda wakashindwa na Waisraeli, kwa hiyo kila mmoja akakimbilia nyumbani kwake.* 23 Mfalme Yehoashi wa Israeli akamkamata Mfalme Amazia wa Yuda, mwana wa Yehoashi mwana wa Yehoahazi,* huko Beth-shemeshi. Kisha akamleta Yerusalemu, naye akabomoa ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu+ mpaka Lango la Pembeni,+ urefu wa mikono 400.* 24 Akachukua dhahabu yote na fedha na vitu vyote vilivyokuwa katika nyumba ya Mungu wa kweli chini ya Obed-edomu na katika hazina za nyumba ya* mfalme,+ na pia akachukua mateka. Kisha akarudi Samaria.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki