-
Isaya 22:20-24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 “‘Siku hiyo nitamwita mtumishi wangu Eliakimu+ mwana wa Hilkia, 21 nami nitamvisha kanzu yako na kumfunga kwa nguvu ukumbuu wako,+ nami nitatia mamlaka yako* mkononi mwake. Naye atakuwa baba kwa wakaaji wa Yerusalemu na nyumba ya Yuda. 22 Nami nitauweka ufunguo wa nyumba ya Daudi+ juu ya bega lake. Atafungua na hakuna yeyote atakayefunga; naye atafunga na hakuna yeyote atakayefungua. 23 Nitampigilia kama kigingi mahali panapodumu, naye atakuwa kama kiti cha ufalme cha utukufu kwa nyumba ya baba yake. 24 Nao watauning’iniza juu yake utukufu* wote wa nyumba ya baba yake, wazao na watoto,* vyombo vyote vidogo, vyombo vyenye umbo la bakuli, na pia mitungi yote mikubwa.
-