-
1 Samweli 29:2-4Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 Na watawala wa Wafilisti walikuwa wakipita wakiwa na vikosi vyao vya mamia na maelfu, naye Daudi na wanaume wake walikuwa wakiwafuata nyuma wakiwa na Akishi.+ 3 Lakini wakuu wa Wafilisti wakauliza: “Waebrania hawa wamekuja kufanya nini?” Akishi akawajibu hivi wakuu wa Wafilisti: “Huyu ni Daudi, mtumishi wa Mfalme Sauli wa Israeli, naye ameishi pamoja nami kwa mwaka mmoja au zaidi.+ Tangu siku aliyokimbilia kwangu mpaka leo sijampata na kosa lolote.” 4 Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia vikali Akishi na kumwambia: “Mrudishe mtu huyu.+ Acha arudi mahali ulipompa. Usimruhusu ashuke kwenda pamoja nasi vitani, asije akatugeuka na kutushambulia wakati wa vita.+ Kuna njia gani bora ya mtu huyu kupata kibali cha bwana wake isipokuwa kumpelekea vichwa vya wanaume wetu?
-