-
Mwanzo 36:31-39Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
31 Sasa hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu+ kabla mfalme yeyote hajawatawala Waisraeli.*+ 32 Bela mwana wa Beori alitawala Edomu, na jiji lake liliitwa Dinhaba. 33 Bela alipokufa, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akaanza kutawala baada yake. 34 Yobabu alipokufa, Hushamu kutoka katika nchi ya Watemani akaanza kutawala baada yake. 35 Hushamu alipokufa, Hadadi mwana wa Bedadi aliyewashinda Wamidiani+ katika eneo* la Moabu akaanza kutawala baada yake, na jiji lake liliitwa Avithi. 36 Hadadi alipokufa, Samla kutoka Masreka akaanza kutawala baada yake. 37 Samla alipokufa, Shauli kutoka Rehobothi karibu na ule Mto akaanza kutawala baada yake. 38 Shauli alipokufa, Baal-hanani mwana wa Akbori akaanza kutawala baada yake. 39 Baal-hanani mwana wa Akbori alipokufa, Hadari akaanza kutawala baada yake. Jiji lake liliitwa Pau, na mke wake aliitwa Mehetabeli binti ya Matredi binti ya Mezahabu.
-