-
2 Samweli 12:30, 31Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
30 Kisha akachukua taji lililokuwa kwenye kichwa cha Malkamu. Uzito wa taji hilo ulikuwa talanta moja* ya dhahabu, nalo lilikuwa na mawe yenye thamani, Daudi akavishwa taji hilo kichwani. Alichukua pia nyara nyingi sana+ kutoka katika jiji hilo.+ 31 Akawatoa nje watu waliokuwa ndani yake, akawapa kazi ya kukata mawe kwa misumeno, vifaa vya chuma vyenye ncha kali na mashoka ya chuma, na kazi ya kufyatua matofali. Hivyo ndivyo alivyofanya katika majiji yote ya Waamoni. Hatimaye Daudi na wanajeshi wote wakarudi Yerusalemu.
-