11 Kwa maana Mfalme Ogu wa Bashani ndiye Mrefaimu pekee aliyekuwa amebaki. Jeneza lake lilitengenezwa kwa chuma,* na bado liko katika jiji la Waamoni la Raba. Lina urefu wa mikono tisa* na upana wa mikono minne, kulingana na kipimo cha kawaida cha mkono.