10 Na Hosa wa wana wa Merari alikuwa na wana. Shimri ndiye aliyekuwa kiongozi, kwa maana ingawa hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimweka kuwa kiongozi, 11 wa pili Hilkia, wa tatu Tebalia, wa nne Zekaria. Wana wote wa Hosa na ndugu zake walikuwa 13.