Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Samweli 23:20-23
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 20 Benaya+ mwana wa Yehoyada alikuwa mwanamume jasiri* aliyefanya mambo mengi ya kishujaa kule Kabzeeli.+ Aliwaua wana wawili wa Arieli wa Moabu, naye aliingia ndani ya shimo la maji siku ya theluji na kumuua simba.+ 21 Alimuua pia mwanamume Mmisri aliyekuwa mkubwa isivyo kawaida. Ingawa Mmisri huyo alikuwa na mkuki mkononi, Benaya alikabiliana naye akiwa na fimbo, akamnyang’anya Mmisri huyo mkuki kutoka mkononi mwake na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe. 22 Benaya mwana wa Yehoyada alifanya mambo hayo, naye alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu hodari. 23 Ingawa alikuwa mashuhuri hata kuliko wale 30, hakuwa shujaa kama wale watatu. Lakini Daudi alimweka kuwa kiongozi wa walinzi wake binafsi.

  • 1 Wafalme 2:35
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 35 Halafu mfalme akamweka Benaya+ mwana wa Yehoyada kuwa mkuu wa jeshi baada yake, na mfalme akamweka Sadoki+ kuwa kuhani badala ya Abiathari.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki