10 Na mfalme wa Babiloni akawachinja wana wa Sedekia huku Sedekia akitazama, na pia akawachinja wakuu wote wa Yuda huko Ribla. 11 Kisha mfalme wa Babiloni akampofusha macho Sedekia,+ akamfunga kwa pingu za shaba, akampeleka Babiloni, na kumfunga gerezani mpaka siku aliyokufa.