-
Kumbukumbu la Torati 6:10-12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 “Yehova Mungu wenu atakapowaleta katika nchi aliyowaapia mababu zenu Abrahamu, Isaka, na Yakobo kwamba atawapa ninyi+—majiji makubwa na yenye kupendeza ambayo hamkujenga,+ 11 nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina mbalimbali ambavyo hamkufanya kazi ili kuvipata, visima ambavyo hamkuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hamkupanda—nanyi mtakapokuwa mmekula na kushiba,+ 12 jihadharini msimsahau Yehova,+ aliyewatoa nchini Misri, kutoka katika nyumba ya utumwa.
-
-
Kumbukumbu la Torati 8:12-14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Baada ya kula na kushiba na kujenga nyumba nzuri na kukaa humo,+ 13 ng’ombe wenu na kondoo wenu watakapokuwa wameongezeka na fedha yenu na dhahabu yenu itakapokuwa imeongezeka na mtakapokuwa na wingi wa vitu vyote, 14 msiache mioyo yenu iwe na kiburi+ na kuwafanya mumsahau Yehova Mungu wenu, aliyewatoa nchini Misri, kutoka katika nyumba ya utumwa,+
-