7 Kwa hiyo tazama! Yehova ataleta dhidi yao
Maji yenye nguvu na yaliyo mengi ya ule Mto,
Mfalme wa Ashuru+ na utukufu wake wote.
Atakuja juu ya sakafu zake zote za vijito
Na kufurika kwenye kingo zake zote
8 Na kupita katika nchi yote ya Yuda.
Atafurika na kuvuka, na kufika shingoni;+
Mabawa yake yaliyonyooshwa yatajaza upana wa nchi yako,
Ewe Imanueli!”+