Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 9:23-26
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 23 Basi alipoingia katika nyumba ya yule mtawala na kuwaona watu waliokuwa wakipiga filimbi na umati uliokuwa na vurugu,+ 24 Yesu akasema: “Ondokeni hapa, kwa maana msichana huyu mdogo hajafa bali amelala usingizi.”+ Ndipo wakaanza kumcheka kwa dharau. 25 Mara tu umati ulipoondolewa, Yesu akaingia na kumshika mkono,+ kisha yule msichana mdogo akainuka.+ 26 Bila shaka, habari hiyo ilienea katika eneo hilo lote.

  • Luka 8:51-56
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 51 Alipofika kwenye nyumba hiyo, hakumruhusu yeyote aingie pamoja naye ila Petro, Yohana, Yakobo, na wazazi wa yule msichana. 52 Lakini watu wote walikuwa wakilia na kujipigapiga kwa huzuni kwa sababu ya yule msichana. Basi akawaambia: “Acheni kulia,+ kwa maana hajafa bali amelala usingizi.”+ 53 Ndipo wakaanza kumcheka kwa dharau, kwa sababu walijua amekufa. 54 Lakini akamshika mkono na kumwita: “Mtoto, inuka!”+ 55 Roho+ yake ikarudi* naye akasimama mara moja,+ kisha Yesu akaagiza apewe chakula. 56 Basi, wazazi wake wakafurahi sana, lakini Yesu akawaagiza wasimwambie mtu yeyote kilichotukia.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki