69 Basi Petro alikuwa ameketi nje katika ua, kijakazi akamjia na kumwambia: “Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mgalilaya!”+70 Lakini akakana mbele yao wote, akisema: “Sijui unachosema.”
69 Yule kijakazi alipomwona akaanza tena kuwaambia wale waliosimama hapo: “Huyu ni mmoja wao.” 70 Petro akakana tena. Baada ya muda mfupi, wale waliosimama hapo wakaanza tena kumwambia: “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana, wewe ni Mgalilaya.”