14 Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimwona mama mkwe wa Petro+ akiwa amelala akiugua homa.+15 Basi Yesu akamgusa mkono,+ naye akapona homa, akasimama na kuanza kumhudumia.
24 Yesu akasema: “Ondokeni hapa, kwa maana msichana huyu mdogo hajafa bali amelala usingizi.”+ Ndipo wakaanza kumcheka kwa dharau. 25 Mara tu umati ulipoondolewa, Yesu akaingia na kumshika mkono,+ kisha yule msichana mdogo akainuka.+