10 Basi Pilato akamuuliza: “Unakataa kuzungumza nami? Je, hujui kwamba nina mamlaka ya kukufungua na mamlaka ya kukuua?” 11 Yesu akamjibu: “Wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Ndiyo maana mtu aliyenitia mikononi mwako ana dhambi kubwa zaidi.”