-
Matendo 18:26-28Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
26 Akaanza kuzungumza kwa ujasiri katika sinagogi, nao Prisila na Akila+ walipomsikia, wakamchukua na kumfafanulia kwa usahihi zaidi njia ya Mungu. 27 Pia, kwa sababu alitaka kuvuka kwenda Akaya, akina ndugu wakawaandikia wanafunzi wakiwahimiza wamkaribishe kwa fadhili. Basi alipofika huko, akawasaidia sana wale ambao kupitia fadhili zisizostahiliwa za Mungu walikuwa wameamini; 28 kwa maana alithibitisha kikamili hadharani na kwa juhudi nyingi kwamba Wayahudi walikuwa wamekosea, na kuwaonyesha kwa Maandiko kuwa Yesu ndiye Kristo.+
-