Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 10/22 uku. 32
  • Lilimfanya Ahisi Afadhali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Lilimfanya Ahisi Afadhali
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 10/22 uku. 32

Lilimfanya Ahisi Afadhali

TARA PATEL huandika safu yenye kichwa “Nikiwa Peke Yangu” katika The Daily, gazeti la habari linalochapishwa katika Bombay, India. Katika Januari aliandika barua kuhusu ile makala “Je, Maisha Yako Ni Makimwa? Waweza Kuyabadili!,” iliyotokea katika Amkeni! la Januari 22, 1995. “Nimeliandikisha,” yeye akasema kuhusu Amkeni!, “ingawa mimi hulifikiria kuwa moja la magazeti yenye maadili bora kupita kiasi ulimwenguni.”

Hata hivyo, yeye aliongezea hivi: “Kwa kuisoma hiyo makala tena na tena, nilijisemea mwenyewe, yakini, maisha yangu ni makimwa, ni makimwa sana. Huwezi kuwazia jinsi yalivyo makimwa! Basi suluhisho ni nini?” Aliendelea kunukuu Amkeni! kwa kina, akimalizia hivi: “Fuliza kujifunza. Uwe na miradi ya kibinafsi. Uwe mbuni. Fanya jambo fulani kwa mikono yako. Uwe na kusudi maishani. Mfikirie Mungu.

“Mashauri yote hayo. Yawe bora kupita kiasi au yasiwe, ukiyafikiria ni ushauri wenye kufaa. Kwa njia fulani gazeti hili la Amkeni hunifanya nijihisi afadhali. Uliandikishe ikiwa unataka.” Kisha Tara Patel akaandaa anwani ya India ili wasomaji waweze kujipatia habari zaidi.

Ikiwa ungependa kupokea nakala ya Amkeni! pamoja na gazeti-jenzi, Mnara wa Mlinzi, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki