Historia ya Mashahidi wa Yehova Katika Nyakati za Kisasa
—United States ya Amerika
JOSEPH RUTHERFORD ndiye aliyejilipia karo ya shule. Kati ya mambo mengine, akawa fundi wa mwandiko wa shorthand, nao ujuzi huu ulimfaa sana miaka mingi baadaye kwa kuandika mawazo ya kutumiwa katika makala zilizohusu Biblia. Alipokuwa shuleni, Joseph Rutherford akawa stenografa (mwandikaji wa shorthand).
J. F. Rutherford baadaye alitumikia miaka minne akiwa wakili wa serikali wa mashtaka katika Bounville, Missouri, Baadaye akawa hakimu wa pekee katika wilaya iyo hiyo iliyoitwa Fourteenth Judicial District of Missouri. Rutherford alikuwa akikaa mahali pa hakimu ikiwa hakimu wa kawaida hakuweza kusimamia mahakma. Maandishi ya mahakma yanaonyesha aliwekwa kuwa hakimu wa pekee zaidi ya mara moja. Kwa hiyo, akapata kuitwa “Judge” (Hakimu) Rutherford.
Hazelle na Helen Krull wanakumbuka walimsikia Rutherford akieleza vile kwanza alivyopendezwa na kweli iliyotangazwa na watumishi wa Yehova. Wanatuambia hivi: “Wakati wa ziara moja yake Ndugu Rutherford alipendekeza tutembee kukiwa na nuru ya mwezi kuelekea sehemu za mashambani. Tulipokuwa tukitembea, alitueleza habari za maisha yake ya kwanza na vile alivyopata kupendezwa na kweli. Alilelewa katika shamba kubwa lakini alitaka kujifunza sheria. Baba yake aliona alipaswa kumsaidia shambani lakini mwishowe akakubali kumwacha aende ikiwa atajilipia karo ya shule na kumlipa pia msaidizi wa shamba atakayefanya kazi humo badala yake. Wakati wa likizo ya wakati wa kiangazi aliuza vitabu ndiyo atimize mapatano yao. . . . Alijiahidi kwamba akiwa wakili mwenye ujuzi angenunua vitabu mtu ye yote akija afisini kwake akiviuza. Siku hiyo ilikuja [mwaka wa 1894], lakini mwanasheria mwenzake ndiye aliyezungumza na aliyefika huko. Alikuwa mwanamke ‘kolpota—Dada Elizabeth Hettenbaugh—naye alikuwa akitoa vitabu vitatu vya Millennial Dawn. Mwenzake hakupendezwa kwa hiyo akamwambia aende [pamoja na kolpota mwenzake, Dada Beeler]. Ndugu Rutherford alimwita arudi baada ya kusikia mazungumzo fulani ya vitabu akiwa katika afisi yake ya faragha, akavichukua vitabu na kuviweka katika maktaba yake nyumbani vikakaa hapo kwa muda fulani. Siku moja alipokuwa akipata nafuu ya ugonjwa alifungua kimojawapo cha vitabu akaanza kukisoma. Huo ulikuwa ndio mwanzo wa kupendezwa maisha yote na utawa na utumishi usiokoma kamwe kwa Mungu wake.”
Mikutano ya Wanafunzi wa Biblia haikufanyiwa katika ujirani wa Rutherford. Walakini, Clarence B. Beaty anasema hivi: “Tangu mwaka wa 1904 na kuendelea, mikutano ilifanyiwa nyumbani mwetu. Dada Rutherford na Hakimu Rutherford walikuja kutoka Boonville, Missouri, kwa ajili ya Ukumbusho [wa mauti ya Kristo]. . . . Alishiriki Ukumbusho wake wa kwanza akatoa hotuba yake ya kwanza ya uhaji kwa marafiki waliokuwamo nyumbani mwetu. Hawakuwa na mtu mwingine ye yote katika kweli huko Boonville.”
Lakini J. F. Rutherford alianzaje kuwa mhubiri wa habari njema? A. H. Macmillan alishiriki sana kumsaidia. Macmillan alimkuta Rutherford mwaka wa 1905 katika Kansas City alipokuwa akisafiri kupitia United States pamoja na Ndugu Russell. Muda mchache baadaye Ndugu Macmillan alitua amtembelee Hakimu Rutherford kwa siku moja au mbili. Katika mazungumzo fulani walisemezana hivi:
“Hakimu, inakupasa uwe ukihubiri kweli hapa.”
“Mimi si mhubiri. Mimi mwanasheria.”
“Sikia Hakimu, nitakuonyesha unaloweza kufanya. Nenda kachukue nakala ya Biblia na kikundi cha watu, na kuwafundisha habari za uzima, mauti na yanayofuata baada yake. Waonyeshe tulikotoa uzima wetu, sababu gani tuliingia katika hali ya kufa na maana ya kifo. Maandiko na yawe shahidi, kisha malizia kwa kusema, ‘Hapo nimetimiza kila jambo kama nilivyosema,’ sawa na vile ungefanya kwa baraza ya mahakimu mahakmani.”
“Kumbe si vigumu sana.”
Jambo gani lilitokea baadaye? Je! Rutherford alifuata shauri hilo? Ndugu Macmillan alieleza habari hizi: “Kulikuwa na mweusi mmoja aliyekuwa akifanya kazi katika shamba dogo lililokuwa karibu na nyumba yake mjini, karibu na pembe ya mji. Karibu weusi kumi na watano au ishirini walikuwako, naye alikwenda huko kuwapa mahubiri juu ya ‘Uzima, Mauti na Yanayofuata Baada Yake.’ Alipokuwa akihutubu wakawa wakisema, ‘Bwana asifiwe, Hakimu! Umejifunza hayo yote wapi?’ Alikuwa na wakati wa kupendeza sana. Hiyo ndiyo iliyokuwa hotuba yake ya kwanza ya Biblia kutoa.”
Muda mfupi baadaye, mwaka wa 1906, J. F. Rutherford alionyesha wakf wake kwa Yehova Mungu. Kaandika Ndugu Macmillan: “Nilikuwa na pendeleo la kumbatiza yeye katika Saint Paul, Minnesota. Alikuwa mmoja wa watu 144 niliobatiza mwenyewe katika maji siku hiyo. Kwa hiyo alipokuwa msimamizi (president) wa Sosaiti, mimi hasa nilipendezwa sana.”
Mwaka wa 1907 Rutherford akawa mshauri wa kisheria wa Watch Tower Society, akitumikia katika makao yake makuu Pittsburg. Alipendelewa kutengeneza mashauri Sosaiti ilipohamisha makao yake kuyapeleka Brooklyn, New York, mwaka wa 1909. Ili afanye hivyo, aliomba akubaliwe katika baraza ya wanasheria wa New York akakubaliwa, akawa wakili mwenye kutambuliwa wa mkoa huo. Mei 24 mwaka uo huo, Rutherford aliruhusiwa pia afanye mazoezi mbele ya mahakma iliyoitwa United States Supreme Court.
J. F. Rutherford alitoa hotuba mara kwa mara akiwa mhaji, mjumbe mwenye kusafiri wa Watch Tower Society. Alisafiri sana akiwa mhutubu wa habari za Biblia katika United States, akihutubu katika vyuo vikuu vingi alipoombwa kufanya hivyo, akahutubia wasikilizaji wengi pia katika sehemu zote za Ulaya. Rutherford alitembelea Misri na Palestina, na mwaka wa 1913 akasafiri Ujeremani akiwa na mkewe, ambako alihutubia jumla ya wasikilizaji 18,000.
—Kutoka 1975 Yearbook of Jehovah’s Witnesses.