Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 7/15 uku. 335
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 7/15 uku. 335

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Je! hapo kwanza Mungu alikusudia mwanamke amtii mumewe? Au ni baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi Mungu alipokusudia iwe hivyo kwa kumwambia mwanamke kwamba “mumeo . . . atakutawala”?​—Mwa. 3:16.

Ni wazi kutokana na maandishi ya Biblia kwamba kusudi la kwanza la Mungu lilikuwa kwamba mwanamume awe kichwa cha jamaa yake naye amtii mumewe.

Kabla Hawa hajaumbwa, Yehova alisema: “Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” (Mwa. 2:18) Kwa hiyo, mwanamume ndiye angekuwa na daraka kubwa katika jamaa naye mwanamke angemsaidia.

Katika 1 Timotheo 2:11-14, mtume Paulo ataja kwamba Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, anapoonyesha kwamba wanawake katika kundi la Kikristo wanapaswa kutii wanaume kama waangalizi na kwamba mwanamke hapaswi “kumtawala mwanamume.” Kwa sababu gani? “Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.”

Ingalimpasa Hawa kuzungumza kwa uangalifu na mumewe kuhusu uamuzi wo wote wa maana uliopaswa kufanywa. Na ingalimpasa kuwa macho kumwomba maoni yake hasa aliposhawishwa ale tunda lililokatazwa, kwa kuwa nyoka alimshawishi asitii amri ambayo Mungu alikuwa amekwisha mpa kupitia kwa mumewe Adamu, kutokula tunda lililokatazwa. Kama angalitambua ukichwa wa mumewe kwa njia hiyo angalikuwa na ulinzi. Kama angalitii ukichwa wake kwa kumwomba maoni yake na kukubaliana naye angalisaidika sana amtolee Mungu ibada ifaayo kwa utii.

Alipokuwa akimhukumu Hawa, Yehova alisema: “Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”​—Mwa. 3:16.

Haionekani kwamba Yehova mwenyewe ndiye aliyeleta hali hizo ziwe adhabu kwa Hawa, kisha mabinti ambao angezaa wazirithi. Bali, kwa kuondoa mwanamke na mwanamume pia katika upendeleo wake, Yehova alikuwa akionyesha mambo mabaya ambayo yangetokea. Kungekuwa na magumu makubwa ya kuzaa watoto chini ya hali za kutokamilika. Yehova alitangulia kujua Kwamba, sasa ndoa ingekuwa mara nyingi na fadhaa, wasiwasi na masumbufu ya kutokamilika. Ingekuwa tamaa ya kawaida mwanamke kutamani mwanamume, si kwa kusudi la kutoshelezwa nyege tu, bali pia kwa sababu ya kutaka nyumba na watoto, ulinzi na ushirika. Tamaa hizo zingekuwa nyingi sana katika mwanamke ingawa angetawalwa na mume asiyekamilika ndipo zitimizwe.

Asingetawalwa na mume kwa njia ya kawaida ya kutumia ukichwa. Nyakati nyingine angetawalwa kwa njia ambayo ingemfanya atake kunyakua ukichwa wa mumewe, naye mwanamume angemzuia asiunyakue. Vilevile, mara nyingi mwanamume angeelekea kutumia vibaya ukichwa wake.

Hata katika ndoa ya Kikristo, mtume Paulo alionya kwamba zingekuwako nyakati za kuwa na “dhiki katika mwili.” (1 Kor. 7:28) Hata hivyo, chini ya hali za kutokamilika, watu wanaweza kupata furaha nyingi na kufanikiwa katika ndoa ya Kikristo. Upendo ukitawala, na mume na mke wakithamini madaraka yao mbalimbali na kuyatimiza, maelekeo yo yote ya mke kujaribu kutawala mumewe au mume kujaribu kutumia vibaya ukichwa wake yangepunguzwa. Mke Mkristo huona hekima ya kutii ukichwa wa mumewe kwa heshima nyingi sana, naye mume Mkristo ajua apaswa kumpenda mkewe kama apendavyo mwili wake mwenyewe.​—Efe. 5:21-23.

Mke Mkristo hana haja ya kujisikia amewekewa vizuizi vya bure kwa sababu ya kutii mumewe ifaavyo. Vivyo hivyo, waliomo katika kundi la Kikristo wanatii wazee wanaoongoza kundi. (Ebr. 13:17) Wazee wana madaraka makubwa zaidi, ingawa si wakubwa kuliko ndugu zao wanaowatumikia. Kwa njia iyo hiyo, mume ana cheo cha kuwa kichwa cha jamaa yake, ingawa hiyo haimfanyi mkubwa kuliko mkewe. Wote wawili watarithi uzima pamoja.​—1 Pet. 3:7.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki