Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 12/1 uku. 3
  • Kutafuta Sana Sifa na Mali Kunaleta Thawabu Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutafuta Sana Sifa na Mali Kunaleta Thawabu Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Habari Zinazolingana
  • Tumaini Lako—Je, Ni Mungu au Mali?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Wewe ‘Umeacha Kuweka Hazina Duniani’?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Mahubiri ya Mlimani—“Jiwekeeni Hazina Mbinguni”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Jinsi Unavyoweza Kupata Mafanikio ya Kweli Maishani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 12/1 uku. 3

Kutafuta Sana Sifa na Mali Kunaleta Thawabu Gani?

ALIKUWA mwimbaji wa umri usiopita miaka 25. Baada ya miaka miwili tu alikuwa amejipatia fedha milioni nyingi. Lakini je! kuwa na sifa na mali kulimletea furaha na uradhi wa kweli?

Mwimbaji huyu aliyependwa na watu wengi alikubali hivi: ‘Sijui kama inafaa kuwa na sifa na fedha. Hata siwezi kwenda katika hoteli nikamaliza kula chakula bila kufuatiwa na wapiga picha, waandikaji wa habari za magazeti pamoja na wale wanaotaka niwape habari za maisha yangu. Ninalazimika kula chakula changu nikiwa katika chumba changu cha hoteli. Siwezi kwenda kutembea kwa sababu ninaweza kutekwa nyara. Siwezi kwenda kutazama sinema au mchezo wa mpira. Yanakuwa maisha ya upweke unapokuwa njiani ukitalii. Unaloweza kufanya peke yake ni kukaa chumbani mwako na kutazama televisioni. Sifungui vifurushi zawadi hata kidogo​—ila tu kutoka kwa rafiki. Huwezi kujua ni kitu gani kinachofungiwa ndani. Huenda likawa kombora lililotumwa na mhalifu fulani.’

Ijapokuwa alikuwa amejulikana na watu wengi na kupata mali nyingi, kijana huyu alikuwa amepoteza mengi. Hangeweza tena kujifurahisha mambo ya kawaida ambayo hakuthamini hapo zamani. Hali yake iliyobadilika ilimfanya kuwa kama mfungwa.

Wengine waliokuwa katika hali zinazofanana na hiyo wamepata kuona ukweli uo huo. Walijitaabisha sana waufikie mradi fulani, baadaye wakaona kwamba haukutimiza mataraja yao. Ijapokuwa walio na mali na sifa huenda wakawa na wengi wawapendao, wana rafiki wa kweli wachache sana. Mara nyingi inatokea kwamba, wakati mtu anapoacha kujulikana na watu wengi na mali inapokwisha, waliompenda wanamgeukia mtu mwingine. Jambo hili la hakika la maisha linakubaliwa na mithali ya kale: “Mali hufanyiza rafiki wengi, bali mtu asiye na mali humpoteza rafiki aliye naye.”​—Mit. 19:4, The New English Bible.

Kwa wazi, kutafuta sifa na mali hakuridhishi. Kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwa habari ya miradi mingine ya mambo ya kimwili, mtu anapaswa kufanya nini kuwa lengo lake kubwa maishani?

Mwanamume ambaye anajulikana sana kuwa ndiye mwalimu mkuu zaidi alishauri hivi: “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba, bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi.”​—Mt. 6:19, 20.

Kwa hiyo, ikiwa tunatamani furaha pamoja na uradhi wenye kuendelea, lazima tuepuke kufanya jambo kubwa maishani mwetu kuwa utafutaji wa mali za kimwili, kwa kuwa hazina thamani (bei) yenye kuendelea na mara nyingi zinakatiza tamaa vibaya sana. Badala yake, tunalopaswa kuhangaikia ni kuwa na msimamo mzuri na Muumba wetu. Akiwa na kumbukumbu letu la matendo mazuri inakuwa kama kwamba tumeweka hazina iliyo salama mbinguni. Hazina hiyo itatuletea zawadi kubwa kutoka kwa Mungu wa milele. Kwa hiyo, badala ya kuwaonea kijicho wale wachache ambao wamepata sifa na mali, tutaridhika kwa kuwa na kitu chenye thamani kubwa zaidi​—uhusiano (urafiki) pamoja na Aliye Juu Zaidi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki