Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 4/15 uku. 24
  • Jina la Yehova—Ni Ulinzi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jina la Yehova—Ni Ulinzi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 4/15 uku. 24

Jina la Yehova—Ni Ulinzi

JINA la Yehova lilikuwa ulinzi kweli kweli kwa shahidi wa Yehova aliyekuwa akitembea kurudi nyumbani usiku sana siku moja akiwa katika barabara yenye giza na isiyo na watu katika Italia. Kama anavyosimulia:

“Ghafula, mwanamume kijana alitokea mbele yangu, akanisimamisha, na kwa sauti yenye kukata maneno akasema: ‘Nimekuvamia. Nipe fedha zote ulize nazo.’ Nikasimama mara moja na mara hiyo ikawa wazi kwangu kwamba hakuwa anacheza; kisha wanaume vijana wengine wanne wa umri wa kuanzia miaka 16 mpaka 18 wakanizunguka wakiwa na visu vyenye kumetameta mikononi mwao. Mara moja nikawapa kibeti changu na, mwingine alipokuwa akichukua fedha zilizokuwa ndani, mwingine alichukua saa yangu na wengine wakachukua vitu nilivyokuwa navyo mifukoni mwangu. Nilipompa mmoja pete yangu ya arusi, alisema hivi: ‘Sitaki hiyo! Hatutachukua hiyo. Badala yake nipe mnyororo mdogo unaozunguka shingo yako.’ Nikamwambia kwamba sivai mnyororo wala hirizi kwa kuwa mimi ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova.

“Nilipomaliza kusema tu mmoja wao nyuma yangu alisema hivi: ‘Tumefanya kosa. Hawa ni watu wazuri. Nawajua.’ Nikamgeukia huyo aliyesema nami nikaanza kumtolea ushuhuda nikimtia moyo aishi kwa unyofu. Nilipokuwa nikisema, ikanistaajabisha, kila mmoja akaanza kurudisha kila alichochukua—mmoja fedha, mwingine saa, mpaka nikarudishiwa kila kitu. Wakaniuliza kama naweza kuwasamehe, nami nikasema kwamba upande wangu hakuna sababu ya kutowasamehe, bali kwamba, mahali pake, wanapaswa kumwomba Yehova awasamehe wakitubu toka moyoni. Nikamshukuru Mungu kwa kunilinda katika pindi hiyo.”

Maneno ya Mithali 18:10, NW ni ya kweli; “Jina la Yehova ni mnara wenye nguvu. Mwenye haki hukimbia ndani yake naye anapewa ulinzi.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki