Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 6/1 uku. 32
  • Hutatamauka

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hutatamauka
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • “Wachukuaji Nuru” Mkusanyiko wa Wilaya wa 1992
    Huduma Yetu ya Ufalme—1992
  • Kwa Nini Wao Hufanya Hivyo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • “Njia ya Mungu ya Maisha” Mkusanyiko wa Wilaya na wa Kimataifa wa 1998
    Huduma Yetu ya Ufalme—1998
  • “Wajumbe wa Amani ya Kimungu” Mkusanyiko wa Wilaya wa 1996
    Huduma Yetu ya Ufalme—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 6/1 uku. 32

Hutatamauka

Wenzi wa ndoa wawili katika Ufilipino walichukua muda wa siku mbili kufika huko. Walitembea kilometa 70, wakiwa wamewabeba watoto wachanga wawili kupitia misitu iliyojaa ruba na kuvuka mito iliyofurika kwa sababu ya tufani. Lakini walipiga moyo konde kutokuukosa.

Wanawake wawili katika Zaire walitembea mwendo wa zaidi ya kilometa 500, wakitumia siku 14 kusafiri, ili kuwa huko. Pia katika Zaire, mwanamume mwenye umri wa miaka 70 alifika huko kwa kuendesha baiskeli yake mwendo wa kilometa 260. Hakuzuiwa na mwendo huo au hali isiyopendeza. Jambo la maana lilikuwa kutokuukosa.

Hao watu wote walikuwa wakienda wapi? Kwenye mojawapo mikusanyiko mikubwa ya Mashahidi wa Yehova iliyopangwa katika nchi zao. Na bila kujali ugumu wa safari, wote walihisi kwamba jitihada zao zilistahili.

Je! umekwisha kufanya mipango ya kuwa kwenye “Wachukuaji Nuru” Mkusanyiko wa Wilaya wa 1992? Yaelekea, hutalazimika kujitahidi sana kama watu wale waaminifu walivyojitahidi ili kuhudhuria. Lakini hata ikiwa inakugharimu uwe na hali zisizopendeza, tunakusihi usiukose.

Programu bora sana na yenye kutumika sana imetayarishwa. Ikiwa unaonea shangwe ushirika wa Kikristo na unapendezwa kujifunza jinsi ya kupata amani ya kweli, lile lililoko katika wakati ujao, au jinsi ya kufanya mapenzi ya Mungu kwa njia bora zaidi, twaweza kuahidi kwamba hutatamauka. Shahidi yeyote katika eneo lako atakuambia mahali na wakati mkusanyiko ulio karibu zaidi na wewe utakapofanywa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki