Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/01 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2001
Huduma Yetu ya Ufalme—2001
km 12/01 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Septemba 3 hadi Desemba 24, 2001. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Kwa kuwa imani ni tunda la roho ya Mungu, watu wasio na imani hawaitafuti roho hiyo, au wanafanya hivyo kwa kusudi lisilofaa au wanakataa itende maishani mwao. (Luka 11:13; Gal. 5:22) [rs-SW uku. 92 fu. 1]

2. Zaburi 58:4 huonyesha kwa usahihi kwamba fira ana ‘masikio’ ambayo hayatumiki kwa sababu yeye ni kiziwi kimaumbile. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona New World Translation of the Holy Scriptures—With References (Rbi8) uku. 1583.]

3. “Jeshi kubwa” la wanawake wanaotajwa kwenye Zaburi 68:11 walikuwa watumwa wa kike wa mataifa ya kigeni ambao waliachiliwa kutoka utekwani wakati wanaume Waisraeli walipoyashinda mataifa ya maadui. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 10/15 uku. 30 fu. 6.]

4. Ikiwa mtu alikuwa amepangiwa siku na jinsi atakavyokufa, hakungekuwa na uhitaji wa kuepuka hali zenye hatari au kujali afya yake, na kujali maonyo ya usalama hakungebadili idadi ya vifo. [rs-SW uku. 28 fu. 2]

5. Paulo alipomwambia Timotheo “usiache kamwe mtu yeyote adharau ujana wako” alimaanisha kwamba Timotheo alikuwa tineja tu au katika miaka yake ya mapema ya 20. (1 Tim. 4:12) [w99-SW 9/15 uku. 29 fu. 1-3; uku. 31 fu. 2]

6. Kama ilivyoandikwa kwenye Zaburi 110:1, “Bwana wangu” ni Yesu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 6/1 uku. 28 fu. 5.]

7. Katika Biblia ya New World Translation, kitabu cha Zaburi hutaja jina Yehova karibu mara 700, na jina lililofupishwa “Yah,” mara 43, kwa hiyo kwa ujumla jina la Mungu latajwa kwa wastani karibu mara 5 katika kila Zaburi. [si-SW uku. 104 fu. 23]

8. Ijapokuwa katika Maandiko Yesu anatajwa kuwa “mungu,” hata “Mungu mwenye nguvu,” hakuna mahali ambapo anatajwa kuwa mweza-yote. (Yn. 1:1; Isa. 9:6; Mwa. 17:1) [rs-SW uku. 222 fu. 10]

9. Kwa kweli, kuchunguza kitabu cha Mithali ni kuchunguza hekima ya Solomoni mwenyewe. [si-SW uku. 106 fu. 1]

10. Shauri la Biblia linalopatikana kwenye Mithali 21:17, la kuepuka ‘kupenda anasa’ laonyesha kwamba ni vibaya kujifurahisha kwa sababu kunafanya mtu akose nafasi ya kufanya mambo ya maana sana. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 10/1 uku. 27 fu. 7.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Karipio la upole la Yesu kwa Martha lilionyesha nini? (Luka 10:40, 41) [w99-SW 9/1 uku. 30 fu. 7]

12. Yehova alimpeleka mtunga-zaburi kwenye “utukufu” gani? (Zab. 73:24) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 12/15 uku. 28 fu. 3.]

13. Mtunga-zaburi ana maoni gani kuhusu mapendeleo ya utumishi kama inavyoonyeshwa kwenye Zaburi 84:1-3? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 3/15 uku. 8 fu. 5-7.]

14. Ufunuo 22:17 na Waroma 2:4, 5 huonyeshaje kwamba Yehova hajui kimbele wala hapangi kimbele kila kitu ambacho watu hufanya? [rs-SW uku. 30 fu. 4-uku. 31 fu. 1]

15. Kwa kuwa Wakristo wa awali waliamini Utawala wa Yesu wa Milenia kama inavyotajwa katika kitabu cha Ufunuo, ni mambo gani yaliyosababisha Wakristo waasi-imani wakatae fundisho hilo la kimungu hatimaye? [w99-SW 12/1 uku. 6 fu. 3–​uku. 7 fu. 5]

16. Wakristo wanapaswa kuweka mipaka gani wanapoangalia “masilahi ya kibinafsi” ya watu wengine? (Flp. 2:4) [w99-SW 12/1 uku. 29 fu. 1]

17. Andiko la Zaburi 128:3 linadokeza nini linapotaja wana kuwa “miche ya mizeituni” inayozunguka meza ya mtu? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w00-SW 8/15 uku. 30 fu. 4.]

18. Tukiiona kazi ya Mungu kuwa yenye kutia kicho, hiyo itatuathirije? (Zab. 139:14) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 10/1 uku. 15 fu. 18.]

19. Kwa nini Mithali 5:3, 4 huongea juu ya matokeo ya ukosefu wa adili kingono kuwa “mchungu kuliko pakanga” na “mkali kama upanga wa makali kuwili”? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w00-SW 7/15 uku. 29 fu. 3.]

20. Kupatana na Mithali 14:29, ufahamu waweza kutusaidiaje twepuke matokeo ya kukosa subira na hasira isiyodhibitiwa? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 3/15 uku. 13 fu. 7-8.]

Andaa neno au maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Manabii wa kweli walisema katika _________________________ na wakajulisha _________________________ . (Kum. 18:18-20; 1 Yoh. 4:1-3) [rs-SW uku. 167 fu. 1, 3]

22. Mithali zina makusudi mawili—_________________________ na kuandaa _________________________ . (Mit. 1:1-4) [w99-SW 9/15 uku. 13 fu. 2]

23. “Mahali pa siri pake Aliye Juu” ni mahali pa _________________________ kwa wale wanaoshikilia upande wa Mungu wa lile suala la _________________________ ; ni “siri,” au hapajulikani, kwa watu _________________________ . (Zab. 91:1) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 12/15 uku. 29 fu. 6.]

24. ‘Kutosahau matendo ya Yehova’ kwahusiana na _________________________ “matendo yake” ya fadhili kama ilivyoelezwa kwenye Zaburi ya 103. (Zab. 103:2, NW) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w99-SW 5/15 uku. 21 fu. 5-6.]

25. Mithali ni usemi wenye nguvu ambao hutumia _________________________ na ambao umekusudiwa _________________________ . [si-SW uku. 107 fu. 6]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Ingawa alikuwa na sababu ya kukasirika kwa sababu ya jinsi alivyotendewa na Sauli, Daudi alijizuia kwa sababu (alitambua kwamba Sauli hakuwa mkamilifu na kwamba lazima watumishi wa Mungu wawe wenye kusamehe; alikumbuka vizuri uhusiano wake na Yehova; alijua kwamba ni kosa kuhukumu wengine). (1 Sam. 24:6, 15) [w99-SW 8/15 uku. 8 fu. 7]

27. (Hekima; Nidhamu; Uadilifu) yahusisha mambo mengi, kutia ndani uelewevu, ufahamu wenye kina, werevu, na uwezo wa kufikiri; (wema; uelewevu; uamuzi mzuri) ni uwezo wa kuchunguza jambo na kupambanua muundo wake kwa kujua uhusiano kati ya sehemu zake mbalimbali na kati ya muundo wote mzima, hivyo kulielewa. (Mit. 1:1-4) [w99-SW 9/15 uku. 13 fu. 3]

28. Yosefu alipata nguvu za kukinza utongozaji wa mke wa Potifa kwa sababu ya (kujua Sheria ya Musa, ambayo ilikataza uasherati; kuheshimu sana cheo kikubwa cha mume wake; kuthamini sana uhusiano wake pamoja na Yehova). (Mwa. 39:7-9) [w99-SW 10/1 uku. 29 fu. 3]

29. Ni wazi kwamba mwandikaji wa Zaburi 119 alithamini sana (neno, au sheria ya Mungu; zawadi ya uhai; taraja la kupata wokovu), ambalo latajwa katika karibu mistari yote ya zaburi hiyo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w99-SW 11/1 uku. 10 fu. 5; w87-SW 3/15 uku. 24 fu. 2.]

30. Katika sura mbili za kwanza za barua ya Paulo kwa (Waroma; Wagalatia; Waebrania), twaona manukuu fulani kutoka Zaburi kuhusu (ubora wa cheo cha; ubatizo wa; huduma ya kidunia ya) Yesu Kristo. [si-SW uku. 105 fu. 28]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Mit. 2:19; 14:15; 18:17; Rom. 10:17; Ebr. 13:18

31. Ili kupata imani, lazima kwanza mtu achunguze kwa uangalifu yale ambayo Biblia inasema. [rs-SW uku.93 fu. 1]

32. Wakristo hawawezi kuendesha biashara zao kwa njia zisizo za haki au ambazo hupuuza masilahi halali ya wengine. [w99-SW 9/15 uku. 10 fu. 2]

33. Huenda wale wanaojiingiza katika ukosefu wa adili kingono wakafikia hatua ambayo hali yao haiwezi kurekebishwa, yaani kifo, ambacho hakiwezi kubadilishwa. [w99-SW 11/15 uku. 27 fu. 4-5]

34. Mtu mwenye hekima na busara huangalia sana matokeo ya matendo yake naye hafuati maelekeo fulani kwa upofu tu eti kwa sababu yanapendwa na wengi. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona g94-SW 12/8 uku. 16 fu. 1.]

35. Hata ingawa hoja ya mtu yaweza kuonekana kuwa ya kweli au sahihi, ni jambo la hekima kusikiliza pande zote mbili kabla ya kufikia uamuzi. [si-SW uku. 111 fu. 36]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki