Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 6/06 uku. 6
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma ya Ufalme—2006
Huduma ya Ufalme—2006
km 6/06 uku. 6

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatashughulikiwa kwa njia ya maswali na majibu katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Juni 26, 2006. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 30 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Mei 1 hadi Juni 26, 2006. [Taarifa: Mahali ambapo vichapo vya marejeo havijaonyeshwa baada ya swali, utahitaji kufanya utafiti wako mwenyewe ili kupata majibu.—Ona Shule ya Huduma, uku. 36-37.]

SIFA ZA USEMI

1. Ubadilifu wa sauti unahusisha nini, na kwa nini hilo ni muhimu? [be uku. 111, masanduku]

2. Tunawezaje kubadili mwendo wetu wa kuzungumza tunapotoa hotuba? [be uku. 112 fu. 3–6, sanduku]

3. Tunawezaje kukuza shauku kwa habari tunayozungumzia, na kwa nini hilo ni muhimu? [be uku. 115 fu. 1–uku. 116 fu. 2, masanduku]

4. Tunapowafundisha wengine, kwa nini ni muhimu kuzungumza kwa hisia, na ni nini kitakachotusaidia kufanya hivyo? [be uku. 118 fu. 2–uku. 119 fu. 5]

5. Eleza umuhimu wa kutumia ishara za mwili na za uso tunapozungumza. (Mt. 12:48, 49) [be uku. 121, masanduku]

HOTUBA NA. 1

6. Ni katika njia gani kitabu cha Ayubu kinamtukuza Yehova na kukazia viwango vyake vya uadilifu vya maisha? [si uku. 100 fu. 39, 41]

7. Ni nini kinachoshuhudia uasilia wa Zaburi? [si uku. 102 fu. 10-11]

8. Linapozungumza kuhusu mtu mwerevu, je, andiko la Methali 13:16 linamfafanua mtu mwenye hila? Eleza. [w04 7/15 uku. 28 fu. 3-4]

9. Roho takatifu hutusaidiaje, na kujua hilo kunapaswa kututia moyo tufanye nini? (Yoh. 14:25, 26) [be uku. 19 fu. 2-3]

10. Yesu anakuja katika maana gani ya ujumla, na kwenye Mathayo 16:28, alikuwa akirejelea kuja kwa njia gani? [w04 3/1 uku. 16 sanduku]

USOMAJI WA BIBLIA WA KILA JUMA

11. Tunaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Ayubu alivyomjibu Yehova kwenye Ayubu 42:1-6?

12. Ni ‘jambo gani la upuuzi’ ambalo mataifa yanaendelea kusema? (Zab. 2:1, 2)

13. Ni misingi gani inayobomolewa? (Zab. 11:3)

14. Mtu mwenye majivuno hupataje “malipo tele”? (Zab. 31:23)

15. Tunaweza kupata kitulizo gani katika Zaburi 40 ambacho kitatusaidia kukabiliana na hali yetu ya kutokamilika inayosababishwa na mwili wetu wenye dhambi na misiba mingine ya mfumo huu wa mambo? (Zab. 40:1, 2, 5, 12)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki