30 ‘Bila shaka wanagawana nyara walizopata,
Msichana mmoja, wasichana wawili, kwa kila shujaa,
Nguo iliyotiwa rangi kwa ajili ya Sisera, nyara ya nguo iliyotiwa rangi,
Vazi lililopambwa, nguo iliyotiwa rangi, mavazi mawili yaliyopambwa
Kwa ajili ya shingo za waliochukua nyara.’