Maelezo ya Chini
a Yasemekana kwamba arithimetiki (usemi unaotokana na neno la Kigiriki linalomaanisha “namba”) ndiyo fani ya hesabu ambayo imekuwepo kwa muda mrefu zaidi. Arithimetiki ilianza kutumiwa maelfu ya miaka iliyopita. Ilitumiwa na Wababiloni, Wachina, na Wamisri wa kale. Arithimetiki hutusaidia kila siku kuhesabu na kupima vitu vilivyopo duniani.