Maelezo ya Chini
a Maandiko yafafanua Lebanoni ya kale kuwa nchi yenye kuzaa sana iliyo na misitu mizuri na mierezi mikubwa, kama ilivyokuwa Bustani ya Edeni. (Zaburi 29:5; 72:16; Ezekieli 28:11-13) Sharoni ilikuwa maarufu kwa sababu ya vijito na misitu yake ya mialoni; Karmeli ilikuwa maarufu kwa sababu ya mashamba yake ya mizabibu, matunda, na miteremko yenye kujaa maua.