Maelezo ya Chini
d Kama inavyoonyeshwa katika 1 Samweli 23:17, Yonathani alisema mambo matano ili kumtia moyo Daudi: (1) Alimsihi Daudi asiogope. (2) Alimhakikishia Daudi kwamba Sauli hangefanikiwa. (3) Alimkumbusha Daudi kwamba atapokea ufalme, kama Mungu alivyoahidi. (4) Aliahidi kwamba atakuwa mshikamanifu kwa Daudi. (5) Alimwambia Daudi kwamba hata Sauli anajua kwamba yeye ni mshikamanifu kwa Daudi.