-
Mwe na Imani Kama ya Abrahamu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
Hivyo Abramu angesuluhishaje ugomvi huo? Alikuwa amechukua Loti baada ya kifo cha baba ya Loti, na labda kumlea kama mtoto wake mwenyewe. Kwa kuwa Abramu ndiye aliyekuwa na umri mkubwa zaidi kati yao wawili, je hakustahili kuchukua kilichokuwa bora zaidi?
11, 12. Abramu alimtolea Loti pendekezo gani la ukarimu, na ni kwa nini uchaguzi wa Loti haukuwa wa hekima?
11 Lakini ‘Abramu akamwambia Loti, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu. Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto.’
-
-
Mwe na Imani Kama ya Abrahamu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
13. Kielelezo cha Abramu chaweza kuwasaidiaje Wakristo ambao huenda wakawa na ugomvi wa kifedha?
13 Lakini Abramu alionyesha imani katika ahadi ya Yehova kwamba hatimaye mbegu yake ingemiliki nchi hiyo yote; hakugombania sehemu ndogo tu ya nchi hiyo. Kwa ukarimu, yeye alitenda kupatana na kanuni ambayo baadaye ilitajwa kwenye 1 Wakorintho 10:24: “Acheni kila mmoja afulize kutafuta sana, si faida yake mwenyewe, bali ya mtu yule mwingine.” Hili ni kikumbusho kizuri kwa wale ambao huenda wakawa na ugomvi wa kifedha na waamini wenzao. Badala ya kufuata ushauri ulio kwenye Mathayo 18:15-17, wengine wamepeleka ndugu zao mahakamani. (1 Wakorintho 6:1, 7) Kielelezo cha Abramu chaonyesha kwamba ni afadhali kupata hasara kifedha badala ya kufanya jina la Yehova lishutumiwe au kuharibu amani ya kutaniko la Kikristo.—Yakobo 3:18.
-