-
Familia ya Yehova Hufurahia Muungano Wenye ThamaniMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
-
-
4. Kwa maneno yako mwenyewe, ungeelezaje yale yanayosemwa na Zaburi 133 kuhusu muungano wa kidugu?
4 Mtunga-zaburi Daudi alithamini sana muungano wa kidugu. Hata alipuliziwa kuimba juu yao! Ebu mwazie akiwa na kinubi chake huku akiimba: “Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja [“muungano,” NW]. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Heremoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka, naam, uzima hata milele.”—Zaburi 133:1-3.
-
-
Familia ya Yehova Hufurahia Muungano Wenye ThamaniMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
-
-
Kuwa kwao pamoja kulikuwa na matokeo mazuri, kama mafuta ya kupaka yenye kuburudisha yaliyokuwa na harufu ya kupendeza. Mafuta hayo yalipomwagwa juu ya kichwa cha Haruni, yalitiririka chini ndevuni mwake na kushuka kwenye ukosi wa vazi lake. Kwa Waisraeli, kuwa kwao pamoja kulikuwa na uvutano mzuri uliopenya kati ya watu hao wote waliokusanyika. Hali za kutoelewana zilisuluhishwa, na muungano uliendelezwa. Muungano huohuo umo katika familia ya Yehova ya tufeni pote leo. Kushirikiana kwa ukawaida kunaleta matokeo mazuri ya kiroho juu ya washiriki wayo. Hali zozote za kutoelewana au magumu yoyote yanaondoshwa kadiri shauri la Neno la Mungu linavyotumiwa. (Mathayo 5:23, 24; 18:15-17) Watu wa Yehova huthamini sana kule kutiana moyo kunakotokana na muungano wao wa kidugu.
-