Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mtumaini Yehova Ukabilipo Janga
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • [Picha katika ukurasa wa 103]

      Isaya aliandamana na Shear-yashubu alipompasha Ahazi ujumbe wa Yehova

  • Mtumaini Yehova Ukabilipo Janga
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 5. Watu wa Mungu leo wafananaje na Isaya?

      5 Yehova amwambia Isaya: “Haya, toka, umlaki Ahazi, wewe na Shear-yashubu mwana wako, huko mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja wa dobi.” (Isaya 7:3) Hebu wazia! Badala ya mfalme kwenda kumtafuta nabii wa Yehova na kuomba mwongozo wake, nabii apaswa kwenda kumtafuta mfalme! Ijapokuwa hivyo, Isaya amtii Yehova kwa utayari. Vivyo hivyo, watu wa Mungu leo huenda kwa utayari kuwatafuta watu waliojawa hofu kwa sababu ya misongo ya ulimwengu huu. (Mathayo 24:6, 14) Yaridhisha kama nini kwamba mamia ya maelfu kila mwaka wanaitikia ziara za wahubiri wa habari njema na kuushika mkono wenye kinga wa Yehova!

      6. (a) Nabii ampasha Mfalme Ahazi ujumbe gani wenye kutia moyo? (b) Ni hali gani iliyopo leo?

      6 Isaya amkuta Ahazi nje ya kuta za Yerusalemu, ambapo mfalme anakagua mifereji ya maji ya jiji, akijitayarishia mazingiwa yanayotarajiwa.

  • Mtumaini Yehova Ukabilipo Janga
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 7. Kwa nini jina la Isaya na la mwanaye yatumainisha?

      7 Katika siku ya Ahazi, ujumbe wa Isaya, maana ya jina la Isaya na pia maana ya jina la mwanawe zawatumainisha wale wanaomtumaini Yehova. Pasipo shaka Yuda imo hatarini, lakini jina Isaya, limaanishalo “Wokovu wa Yehova,” huashiria kwamba Yehova atawakomboa. Yehova amwambia Isaya aandamane na Shear-yashubu mwanawe, ambaye jina lake lamaanisha “Mabaki Wachache Tu Ndio Watakaorudi.” Hata ufalme wa Yuda uangukapo hatimaye, Mungu atawarudisha mabaki kwa rehema kwenye nchi hiyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki