Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Babeli Umeanguka”!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 5. Babiloni apataje sifa ya kuwa mwenye ‘kutenda hila’ na “mharibu”?

      5 Katika siku ya Isaya, Babiloni bado haijawa serikali kubwa ya ulimwengu, lakini tayari Yehova aona kimbele kuwa wakati wake ufikapo, itatumia mamlaka yake kwa njia mbaya. Isaya aendelea: “Nimeonyeshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu.” (Isaya 21:2a) Kwa hakika Babiloni ataharibu na kutenda hila dhidi ya mataifa anayoyashinda, kutia ndani Yuda. Wababiloni watateka Yerusalemu nyara, wapore hekalu lake, na kuchukua watu wake mateka hadi Babiloni. Wakiwa huko, mateka hao wasio na uwezo watatendewa hila, watadhihakiwa kwa sababu ya imani yao, nao hawatapewa tumaini lolote la kurudi nchini kwao.—2 Mambo ya Nyakati 36:17-21; Zaburi 137:1-4.

      6. (a) Yehova atakomesha huzuni gani? (b) Ni mataifa gani yaliyotabiriwa yatashambulia Babiloni, na hilo latimizwaje?

      6 Naam, Babiloni astahili kabisa hayo “maono magumu,” yatakayomsababishia magumu. Isaya aendelea: “Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote.” (Isaya 21:2b) Wale wanaoonewa na milki hiyo yenye hila watapata kitulizo. Hatimaye, huzuni yao itakoma! (Zaburi 79:11, 12) Kitulizo hicho kitakujaje? Isaya ataja mataifa mawili yatakayoshambulia Babiloni: Elamu na Umedi. Karne mbili baadaye, mwaka wa 539 K.W.K., Koreshi Mwajemi ataongoza jeshi la mwungano wa Waajemi na Wamedi dhidi ya Babiloni. Kwa habari ya Elamu, watawala wa Uajemi watamiliki angalau sehemu ya nchi hiyo kabla ya mwaka wa 539 K.W.K.a Basi, majeshi ya Uajemi yatatia ndani Waelami.

  • “Babeli Umeanguka”!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Nyakati nyingine Mfalme Koreshi wa Uajemi aliitwa “Mfalme wa Anshani”—Anshani lilikuwa eneo au mji katika Elamu. Huenda Waisraeli wa siku ya Isaya—karne ya nane K.W.K.—hawakufahamu Uajemi, ingawa labda walijua Elamu. Huenda hilo likaeleza sababu Isaya hapa ataja Elamu badala ya Uajemi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki