-
Yehova Aharibu Kiburi cha TiroUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
6. Eleza uhusiano uliopo baina ya Tiro na Sidoni.
6 Watu wa pwani ya Foinike pia watavunjika moyo. Nabii asema: “Tulieni, enyi mkaao kisiwani [“pwani,” “NW”]; wewe ambaye wafanya biashara wa Sidoni, wavukao bahari, walikujaza.
-
-
Yehova Aharibu Kiburi cha TiroUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
‘Wakazi wa pwani’—jirani za Tiro—watakaa kimya wakishangaa sana juu ya maafa ya kuanguka kwa Tiro. “Wafanya biashara wa Sidoni” ambao ‘wamewajaza’ wakazi hao, wakiwafanya matajiri, ni kina nani? Hapo awali Tiro lilikuwa koloni la jiji la pwani liitwalo Sidoni, ambalo lilikuwa kilometa 35 tu upande wa kaskazini. Kwenye sarafu zake, Sidoni lajiita mama ya Tiro. Ingawa mali za Tiro zimeshinda za Sidoni, hilo lingali “binti wa Sidoni,” na wakazi wake wangali wajiita Wasidoni. (Isaya 23:12) Kwa hiyo, yaelekea usemi “wafanya biashara wa Sidoni” wawarejezea wafanya-biashara wakazi wa Tiro.
-