Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Aharibu Kiburi cha Tiro
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 19, 20. Ni nani anayetabiriwa kuwa atashinda Tiro, na unabii huo watimizwaje?

      19 Ni serikali gani itakayotekeleza hukumu ya Yehova juu ya Tiro? Isaya atangaza: “Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha buruji zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.

  • Yehova Aharibu Kiburi cha Tiro
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 23:13,

  • Yehova Aharibu Kiburi cha Tiro
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Wakaldayo—wala sio Waashuri—ndio watakaoshinda Tiro. Watasimamisha buruji zao za mazingiwa, wayaharibu majumba ya enzi ya Tiro, na kuifanya hiyo ngome ya meli za Tarshishi kuwa magofu yanayobomoka.

      20 Kwa utimizo wa unabii huo, muda mfupi baada ya kuanguka kwa Yerusalemu, Tiro laasi dhidi ya Babiloni, na Nebukadreza azingia jiji hilo. Tiro lakabili mazingiwa hayo, likiamini kwamba haliwezi kushindwa. Mazingiwa yaendeleapo, wakuu wa majeshi ya Babiloni watiwa ‘upaa vichwani’ kutokana na mkwaruzo wa kofia zao za chuma na mabega yao ‘yaambuliwa ngozi’ kutokana na kubeba vifaa vinavyotumiwa katika ujenzi wa mazingiwa. (Ezekieli 29:18) Mazingiwa hayo yamgharimu sana Nebukadreza. Jiji la Tiro barani laharibiwa, ingawa Nebukadreza haiteki nyara yake. Hazina nyingi za Tiro zimehamishiwa kwenye kisiwa kidogo kilichoko karibu meta 800 kutoka pwani. Kwa kuwa hana kundi la meli, mfalme huyo wa Wakaldayo ashindwa kuteka kisiwa hicho. Tiro lasalimu amri baada ya miaka 13, ingawa litasalia na lione utimizo wa unabii mwingine mbalimbali.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki