-
Yehova Ni MfalmeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.
-
-
Yehova Ni MfalmeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
7. Agano la Sheria lingekuwaje baraka kwa Waisraeli?
7 Miaka ipatayo 800 kabla ya siku ya Isaya, Waisraeli walifanya uhusiano wa agano na Yehova kwa hiari, nao wakakubali kushikamana nalo. (Kutoka 24:3-8) Masharti ya agano la Sheria yalisema kuwa iwapo wangetii sheria za Yehova, wangepata baraka zake tele lakini iwapo wangekiuka agano hilo, wangepoteza baraka zake na adui zao wawatwae mateka. (Kutoka 19:5, 6; Kumbukumbu la Torati 28:1-68) Agano hilo la Sheria, lililotolewa kupitia Musa, lingetumika kwa muda usio dhahiri. Lingewalinda Waisraeli hadi kufika kwa Mesiya.—Wagalatia 3:19, 24.
8. (a) Watu ‘wameziasije sheria’ na ‘kuibadili amri’? (b) “Wakuu” wanakuwa wa kwanza ‘kudhoofika’ kwa njia zipi?
8 Lakini watu “wamelivunja agano la milele.” Wameziasi sheria za Mungu, wakizipuuza. “Wameibadili amri,” wakifuata mazoea ya sheria tofauti na zile ambazo Yehova alitoa. (Kutoka 22:25; Ezekieli 22:12)
-