Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mfalme na Wakuu Wake
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Tetemekeni, enyi wanawake wenye raha; taabikeni, enyi msiokuwa na uangalifu.” (Isaya 32:9-11a) Mtazamo wa wanawake hao huenda ukatukumbusha watu wanaodai kumtumikia Mungu leo bali hawana bidii katika utumishi wake. Watu hao wamo katika “Babiloni Mkubwa, mama wa makahaba.” (Ufunuo 17:5) Kwa kielelezo, washiriki wa dini za Jumuiya ya Wakristo wanafanana sana na jinsi Isaya anavyowafafanua “wanawake” hao. Wana “raha,” pasipo kujali hukumu na fadhaiko ambazo zitawaangamiza karibuni.

      18. Ni nani anayeagizwa ‘ajivike viuno nguo za magunia,’ na kwa nini?

      18 Basi, dini isiyo ya kweli yatolewa mwito: “Jivueni, jivueni nguo zenu kabisa, jivikeni viuno nguo za magunia.

  • Mfalme na Wakuu Wake
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 32:11b

  • Mfalme na Wakuu Wake
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Yaelekea usemi “Jivueni, jivueni nguo zenu kabisa” haumaanishi kuvua nguo zote na kubaki uchi. Watu wa kale walikuwa na desturi ya kuvaa vazi la nje juu ya vazi la ndani. Mara nyingi vazi la nje lilimtambulisha mtu. (2 Wafalme 10:22, 23; Ufunuo 7:13, 14) Kwa hiyo, unabii huo unawaamuru washiriki wa dini zisizo za kweli wavue nguo zao za nje—utambulisho wao bandia wa kuwa watumishi wa Mungu—na badala yake wavae nguo za magunia, zinazofananisha kuombolezea hukumu yao iliyo karibu. (Ufunuo 17:16)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki