Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Aghadhibikia Mataifa
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 12. (a) Yehova atumia nani kuleta adhabu dhidi ya Edomu? (b) Nabii Obadia atabiri nini kuhusu Edomu?

      12 Mungu akusudia kuiadhibu Edomu kwa sababu ya matendo yenye nia mbaya dhidi ya tengenezo Lake la duniani, liitwalo Sayuni. Unabii wasema: “Ni siku ya kisasi cha BWANA, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.” (Isaya 34:8) Muda mfupi baada ya uharibifu wa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K., Yehova aanza kuonyesha kisasi chake chenye haki juu ya Waedomi kupitia Nebukadreza, mfalme wa Babiloni. (Yeremia 25:15-17, 21) Majeshi ya Babiloni yavamiapo Edomu, hakuna kiwezacho kuwaokoa Waedomi! Ni “mwaka wa malipo” dhidi ya nchi hiyo yenye milima mingi. Yehova atabiri kupitia nabii Obadia: “Kwa sababu ya udhalimu aliotendwa ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele. . . . Kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.”—Obadia 10, 15; Ezekieli 25:12-14.

  • Yehova Aghadhibikia Mataifa
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Wakati Ujao Usio na Matumaini kwa Jumuiya ya Wakristo

      13. Ni nani aliye kama Edomu leo, na kwa nini?

      13 Leo, kuna tengenezo ambalo mambo yake ni kama ya Edomu. Ni tengenezo gani hilo? Ni nani leo wamekuwa kwenye mstari wa mbele kutukana na kunyanyasa watumishi wa Yehova? Je, si Jumuiya ya Wakristo, kupitia jamii yake ya makasisi? Ndiyo! Jumuiya ya Wakristo imejiinua kufikia mahali pa juu kama mlima katika mambo ya ulimwengu huu. Hiyo ina cheo cha juu katika mfumo wa mambo wa wanadamu, na dini zake ni sehemu kubwa ya Babiloni Mkubwa. Lakini Yehova ameamuru kuwepo “mwaka wa malipo” dhidi ya Edomu hii ya leo kwa sababu ya tabia yake mbaya ya jeuri kuelekea watu Wake, Mashahidi Wake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki